1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANTANANARIVO: Uchaguzi wa rais nchini Madagaskar

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCn6

Uchaguzi wa rais unafanywa hoo leo katika kisiwa cha Madagaskar kwenye Bahari ya Hindi.Wagombeaji 14 wanagombea cheo cha rais katika kisiwa kikubwa cha nne duniani,ambacho tangu mwaka 2002 kinaongozwa na Marc Ravalomanana.Kufuatana na uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni, kiongozi huyo anatazamiwa kushinda uchaguzi wa leo.Mshindi atahitaji kujichotea zaidi ya asili mia 50 ya kura ili kuzuia duru ya pili ya uchaguzi.Milionea Ravalomanana alietajirika kwa biashara ya maziwa,anagombea awamu ya pili akitaka kuendelea na mageuzi ya kiuchumi katika dola lililo miongoni mwa nchi masikini kabisa duniani.Upinzani mkali unatazamiwa kutoka upande wa mwanasiasa mkongwe Norbert Lala Ratsirahonana aliewahi kuwa waziri mkuu nchini humo.