1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANTANANARIVO: Wapiga kura waamuwa kumpa rais uwezo zaidi

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAl

Wapiga kura katika visiwa vya Madagascar wamepitisha kwa wingi pendekezo la kufanya marekebisho ya katiba ili kumpa uwezo mkubwa rais wa nchi hiyo na wakati huo huo kutumiwa lugha ya kiingereza kama lugha rasmi katika nchi hiyo iliyokuwa koloni la Ufaransa.

Matokeo yameonyesha kuwa asilimia 75.38 ya watu wamepiga kura ya kuunga mkono mabadiliko hayo.

Hata hivyo matokeo hayo lazima yaidhinishwe na mahakama ya katiba.

Wanachama wa upinzani wamedai kuwa kura hiyo ilikabiliwa na visa vya udanganyifu.