1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Antonio Conte kuchukua usukani Chelsea

4 Aprili 2016

Antonio Conte amepewa jukumu la kuyafufua mafanikio ya Chelsea na kuleta taji la ligi ya Premier katika uwanja wa Stamford Bridge baada ya kutangazwa leo kuwa kocha wao mpya

https://p.dw.com/p/1IPEI
Fußball Länderspiel Deutschland - Italien
Picha: Reuters/M. Rehle

Muitaliano Conte, mwenye umri wa miaka 46 ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Italia, atahamia London kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya dimba la mataifa ya Ulaya – Euro 2016 litakaloanza Juni 10 – Julai 10 nchini Ufaransa.

Conte kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kuwa chaguo la kwanza la Chelsea kumrithi Jose Mourinho kama kocha wao wa kudmu kufuatia kutimuliwa kwa Mreno huyo mwezi Desemba baada ya Chelsea kuwa na mwanzo wao mbaya kabisa katika msimu wa ligi kuu katika zaidi ya miaka 30.

Conte atakuwa kocha wa tano Muitaliano kuifunza Chelsea, baada ya Gianluca Vialli, Claudio Ranieri, Carlo Ancelotti na Roberto Di Matteo. Alichezea Juventus zaidi ya mechi 400 na akaifunza klabu hiyo ambapo alishinda mataji matatu mfululizo ya Serie A kaunzia 2012 hadi 2014.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri:Yusuf Saumu