1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Vyombo vya habari

"App" ya DW kwenye simu yako

17 Desemba 2015

Sasa unaweza kupokea taarifa, habari, makala na mengi mengineyo moja kwa moja na tena bila malipo kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW kupitia simu yako ya mkononi ama tablet kwa kutumia "App" ya DW.

https://p.dw.com/p/1G70J
App mpya ya DW Kiswahili
App mpya ya DW KiswahiliPicha: DW

Ipate App mpya ya DW kupitia iTunes App Store au Google Play Store. Ukishapakua App yako kwa lugha ya Kiingereza, unaweza kubadili kwa lugha ya Kiswahili kwa kufuata hatua zifautazo:

- Bonyeza misitari mitatu iliyoko pembeni mwa nembo ya DW upande wa juu kushoto - Itakuletea „Top Stories“.

- Bonyeza settings chini kabisa

- Bonyeza „Language“

- Bonyeza Kiswahili na kisha,

- Restart Now