1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arab league wasema Gaza isaidiwe kutokana na kufungwa mipaka yake na Israel

21 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvZM

CAIRO:

Maofisa wa jumuia ya nchi za kiarabu-Arab League-wamekusanyika mjini Cairo katika kikao cha dharura ili kujadilia mzingiro wa Ukanda wa Gaza uliowekwa na Israel siku nne zilikizopota.Israel imechukua hatua hiyo kufuatia uvurumishwaji wa maroketi unaofanywa na wa Palestina.

Mtambo pekee wa kuzalisha umeme wa Gaza uliishiwa mafuta jumapili,na kusababisha giza na hivyo kuathiri bekeri za mikate pamoja na zahanati. Wakazi wa Gaza, wanaofikia miliioni moja Unusu, wanategemea misaada.Shirika linalohudumia wakimbizi wa Palestina la Umoja wa Mataifa- limeielezea hali katika ukanda wa Gaza kama janga la kibinadamu.Lakini maofisa wa serikali ya Israel wamekanusha hilo wakisema kuwa Gaza baado ina chakula pamoja na nishati vya kutosha.Aidha wamekariri mwito kwa kundi la Hamas,linalodhibiti Gaza kukomesha uvumrumishaji wa maroketi katika maeneo ya kusini mwa Israel.Mvutano ulizidi jumanne ya wiki jana, na kulilazimisha jeshi la Israel kujibiza mipigo na hivyo kuwauwa waPalestina 19. Israel iliondoka kutoka maeneo hayo mwaka wa 2005 ,lakini baado inadhibiti mipaka ya Gaza pamoja na misaada kadhaa.