1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Armenia, Azerbaijan zakubali kubadilishana wafungwa

Lilian Mtono
8 Desemba 2023

Armenia na Azerbaijan wamekubaliana hapo jana kubadilishana wafungwa wa kivita na kushirikiana ili hatimaye kusainiwa makubaliano ya amani.

https://p.dw.com/p/4ZuYO
Arayik Harutyunyan, kiongozi wa zamani wa mkoa wa Nagorno-Karabakh (katikati) baada ya kutiwa nguvuni na vyombo vya usalama vya Azerbaijan mwezi Oktoba 2023.
Arayik Harutyunyan, kiongozi wa zamani wa mkoa wa Nagorno-Karabakh (katikati) baada ya kutiwa nguvuni na vyombo vya usalama vya Azerbaijan mwezi Oktoba 2023.Picha: AP Photo/picture alliance

Umoja wa Ulaya umeisifia hatua hiyo kubwa inayoashiria kupatikana kwa amani katika eneo hilo lenye mzozo wa muda mrefu.

Mataifa hayo mawili yamesema kwenye taarifa yao ya pamoja kwamba wanaamini ipo fursa ya kihistoria ya kufikia makubaliano ya amani yaliyosubiriwa kwa muda mrefu.

Soma zaidi: Azerbaijan yataka mazungumzo ya amani na Armenia bila muingilio wa Magharibi

Wamesema wananuwia kurejesha mahusiano katika hali ya kawaida na kupata makubaliano ya amani kwa msingi wa kuheshimu kanuni za uhuru na uadilifu wa kila taifa.

Armenia aidha imekubali kuondoa pingamizi lake dhidi ya Azerbaijan kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa mwaka ujao kuhusu mabadiliko ya tabianchi, kama sehemu ya makubaliano hayo.