1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA: Kesi ya mauaji ya halaiki ya Rwanda imeanza leo

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcK

Kesi dhidi ya afisa wa Rwanda anayetuhumiwa kuwa miongoni mwa watu waliohusika kupanga mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 imeanza kusikilizwa leo jkatika mahakama ya Umoja wa Matafia ya jinai mjini Arusha Tanzania.

Tharcisse Renzaho, gavana wa zamani wa mji mkuu, Kigali, ameshtakiwa kwa mauaji ya halaiki, kukubali kushiriki katika mauaji hayo, mauji kama uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauaji kama uhalifu wa kivita na ubakaji.

Waongozaji mashataka wa mahakama ya mjini Arusha wamezingatia kile wanachokiita kuhusika moja kwa moja kwa Renzhao katika kuwaua watutsi wakati wa mauaji ya halaiki yaliyosababisha vifo vya watu 800,000.