1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA.Padri wa kanisa katoliki ahukumiwa

13 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjh

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia mauaji ya halaiki ya nchini Rwanda yenye makao yake mjini Arusha nchini Tanzania, imemuhukumu padri wa kikatoliki kwa mchango wake katika mauaji hayo ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Mchungaji Athanase Seromba ndio padri wa kwanza kuhukumiwa na mahakama hiyo akipewa kifungo cha miaka 15 baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili kati ya manne yaliyomkabili.

Seromba wa kabila la Hutu alikabiliwa na mashtaka yaliyohusiana na kuamrisha kubomolewa kanisa lililokuwa chini ya uongozi wake wakati raia 2000 wa kabila la Watutsi wakiwa ndani ya kanisa hilo kujihifadhi mwezi April mwaka 1994.

Raia wote hao waliuwawa, akijitetea mchungaji Athanase Seromba aliiambia mahakama kwamba yeye alikuwa ni mchungaji tu na wala hangeweza kuzuia mauaji hayo.