1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA:Waasi wa Darfur wakutana kufikia muafaka na serikali

3 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcZ

Makundi ya waasi ya Darfur nchini Sudan wanakutana mjini Arusha nchini Tanzania kwa mazungumzo yanayolenga kufikia mwafaka kufuatia hatua ya kuidhinisha azimio la Umoja wa mataifa la kuepeleka kikosi cha kulinda amani kilichoimarishwa kwenye eneo la Darfur.

Mkutano huo unafadhiliwa na Umoja wa Afrika pamoja na Umoja wa Mataifa na unaazimia kuwashawishi waasi kufanya mazungumzo ya amani na serikali ya Sudan.

Makubaliano ya Darfur kati ya serikali na waasi yalifikiwa mwaka jana lakini kuidhinishwa na kundi moja tu kati ya makundi matatu yanayojadiliana na serikali.