1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASEAN na Umoja wa Ulaya wataka demokrasia Myanmar

Maja Dreyer22 Novemba 2007

Nchi za Umoja wa Ulaya na za jumuiya ya Kusini Mashariki mwa Asia, zilitoa mwito wa pamoja kuleta demokrasia Myanmar na kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa miongoni mwa kiongozi wa upinzani Bibi Aung San Su Kyi.

https://p.dw.com/p/CS1v
Maandamano Myanmar mwezi wa Septemba yalikandamizwa
Maandamano Myanmar mwezi wa Septemba yalikandamizwaPicha: AP

Ukiukaji wa haki za binadamu nchini Myanmar ulikuwa mada muhimu kwenye mkutano uliofanyika leo kati ya viongozi wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia na wajumbe wa Umoja wa Ulaya. Hata makubaliano juu ya biashara huyu kati ya jumuiya hizo mbili yalikwama kutokana na suala hilo la kudai mageuzi huko Myanmar ambayo iliwekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya wiki hii. Kile kilichokubaliwa ni mwito wa kudai wafungwa wa kisiasa waachiliwe huyu, kama alivyothibitisha mkuu wa tume ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso. Barroso aliongeza: “Katika masuala ya haki za binadamu tunakaribianan. Lakini tunaunga mkono utaratibu wa kutafuta maridhiano ya kitaifa huko Myanmar.”


Wajumbe wa Umoja wa Ulaya lakini walitetea hatua zao za kuiwekwa vikwazo Myanmar. Umoja huu unazuia biashara ya makampuni 1200 ya Myanmar pamoja na kuongeza muda wa kupiga marufuku visa na vikwazo kwa amana za benki za viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo. Hii imekuja baada ya serikali ya Myanmar kukandamizi kwa nguvu maadamano ya kudai demokrasia hapo mwezi wa Septemba.


Nchi za jumuiya ya ASEAN lakini zinapinga vikwazo hivyo. Hata hivyo, baada ya kukubali takwa la Myanmar na kufuta mwaliko kwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa Ibrahim Gamhari kuzungumza mbele ya mkutano huu, sasa waziri mkuu wa Singapur Lee Hsien Long amechukua msimamo wa kustaajabisha wa kuitaka Myanmar kuharakisha juhudi za kuleta masikizano ya taifa: “Maana ya masikizano ya kitaifa ni kuanzisha mazungumzo na Aung San Su Kyi na chama chake, yana maana kuwaacha huru wafungwa wa kisiasa pamoja na Aung San Su Kyi. Yana maana kutafuta njia ya amani kugeukia demokrasia na kumaliza kuwanyonya wananchi kiuchumi. Kwa maoni ya viongozi wengi wa jumuiya ya ASEAN ni wazi nini lazima kifanywe.”


Lakini nchi za ASEAN hazikubaliani juu ya hayo. Kulingana na wachunguzi wasio wa upande mmoja, hilo ndilo tatizo la jumuiya hiyo yenye mataifa yaliyo na mifuno na dini tofauti.


Masuala mengine yaliyozungumziwa ni bei ya mafuta ambayo kiwango chake cha juu kinawatia wasiwasi viongozi wa jumuiya zote mbili za Ulaya na Asia. Vilevile walizungumzia utunzaji wa hali ya hewa na mkutano utakaofanyika Bali mwezi ujao.