1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ashton akutana na Mursi

30 Julai 2013

Mwanadipomasia wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amekutana kwa muda wa saa mbili na rais aliyeondolewa madarakni nchini Misri Mohammed Mursi.

https://p.dw.com/p/19H2d
Egypt's interim President Adli Mansour (R) meets with EU foreign policy chief Catherine Ashton at El-Thadiya presidential palace in Cairo July 29, 2013. Ashton became the first senior overseas envoy to visit Egypt's new rulers since the weekend killing of at least 80 supporters of the country's deposed Islamist president. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh (EGYPT - Tags: POLITICS)
Catherine Ashton (kushoto) akizungumza na rais wa mpito Adli Mansour mjini CairoPicha: Reuters/Amr Abdallah Dalsh

Hayo yameelezwa leo(30.07.2013) na Umoja wa Ulaya, ikiwa ni mkutano wa kwanza wa kiongozi huyo anayeelemea zaidi itikadi za dini ya Kiislamu na kiongozi kutoka nje ya nchi hiyo tangu pale jeshi la Misri lilipomuondoa madarakani karibu mwezi mmoja uliopita.

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton alikutana na Morsi jana jioni(29.07.2013) , kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika ukurasa wa Twitter na msemaji wa Ashton, Maja Kocijancic. Hakusema hata hivyo mkutano huo ulifanyika wapi, na hakutoa maelezo ya majadiliano hayo.

EU foreign policy chief Catherine Ashton attends a meeting with Egypt's interim President Adli Mansour (not seen) at El-Thadiya presidential palace in Cairo, July 29, 2013. Ashton became the first senior overseas envoy to visit Egypt's new rulers since the weekend killing of at least 80 supporters of the country's deposed Islamist president. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh (EGYPT - Tags: POLITICS)
Catherine AshtonPicha: Reuters

Mursi hajulikani aliko

Tangu mapinduzi ya Julai 3, ambayo yalifuatia maandamano makubwa ya mamilioni ya Wamisri wakitaka kuondolewa madarakani kwa Mursi, rais huyo wa zamani amekuwa akishikiliwa mahali pasipojulikana na jeshi bila mawasiliano na watu kutoka nje. Kundi la wanaharakati wa haki za binadamu nchini Misri lilichukuliwa na wanajeshi hadi mahali ambapo Mursi anashikiliwa na jeshi wiki hii lakini alikataa kuonana nao.

Waendesha mashitaka siku ya Ijumaa wamesema Mursi anakabiliwa na mashtaka ya kushirikiana na kundi la wapiganaji wa Kipalestina wa Hamas na kutoroka kutoka jela wakati vuguvugu wa maandamano ya umma mwaka 2011 na kuuangusha utawala wa kimabavu wa Hosni Mubarak.

Ashton yuko nchini Misri katika ziara yake ya pili mwezi huu kutafuta njia za kuitoa Misri katika umwagaji damu pamoja na mzozo wenye utata, akitafuta maridhiano katika mazungumzo na serikali inayoungwa mkono na wanajeshi pamoja na washirika wa rais aliyeondolewa madarakani.

epa03764865 Egyptian activists gather in support of Egyptian President Mohammed Morsi during a pro-government rally in Cairo, Egypt, 28 June 2013. Supporters of Morsi rallied two days ahead of mass protests planned by opposition groups to call on the Islamist leader to step down. EPA/KHALED ELFIQI +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wamisri waendelea na maandamanoPicha: picture-alliance/dpa

Ashutumu mauaji

Kabla ya ziara yake , Ashton alishutumu ghasia zilizotokea mwishoni mwa juma ambapo watu 83 waliuwawa wakati wa maandamano na alitoa wito wa kufanyika hatua za kisiasa ambazo zitajumuisha makundi yote, ikiwa ni pamoja na kundi la Udugu wa Kiislamu la Mursi.

Lakini hakuna dalili kuwa kila upande wa mzozo huo uko tayari kukubaliana na miito yake. Kundi la Udugu wa Kiislamu limekataa wito wa kufanyakazi pamoja na viongozi wapya na kuitisha maandamano mapya leo. Serikali nayo haikutoa ishara ya kuleta maridhiano.

U.S. Secretary of State John Kerry speaks about Syria at a news conference with Qatar's Prime Minister Sheikh Hamad bin Jassim al-Thani (unseen) in Doha June 22, 2013. Kerry said the meeting of 11 countries in Qatar was a chance to discuss "efforts to increase and coordinate support for the Syrian political and military opposition". REUTERS/Jacquelyn Martin/Pool (QATAR - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John KerryPicha: Reuters

Ziara ya Ashton na mazungumzo ya simu kati yake na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry pamoja na viongozi wa Misri yanaonesha hali ya jumuiya ya kimataifa kuona umuhimu wa kuchukua hatua za haraka, ambapo viongozi wake wanahimiza zaidi hatua za kisiasa ambazo zitajumuisha makundi yote hatua ambazo zitamaliza ghasia.

Kundi la Udugu wa Kiislamu na washirika wake linadai kuwa Mursi ni lazima arejeshwe madarakani, lakini serikali inayoungwa mkono na jeshi inataka kuendelea mbele na mpango wake wa mpito ambao utaelekeza katika uchaguzi wa bunge na rais mapema mwakani.

Wakati huo huo jeshi la Misri limesema limechunguza ripoti kuwa kulikuwa na mripuko katika eneo la mfereji wa Suez lakini ripoti hizo si za kweli na halikupata ushahidi wa tukio hilo.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman