1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Askari mtoto afikishwa mahakamani Guantanamo

10 Agosti 2010

Leo hii, katika jela ya Marekani ya Guantanamo, inasikilizwa kesi nyingine dhidi ya mfungwa anaeshukiwa ugaidi.

https://p.dw.com/p/Ohr1
** FILE ** This is a photo of Omar Khadr, taken before he was imprisoned, handed out by his mother Maha Khadr following a news conference in Toronto on Feb. 9, 2005. A military judge on Monday dismissed charges against Canadian detainee Omar Khadr, saying the matter is outside the jurisdiction of the new military tribunal system. The dismissal of the charges does not mean he will be freed from Guantanamo. (AP Photo/Family Handout via Canadian Press)
Picha ya Omar Khadr kabla ya kutiwa jela, iliyotolewa na mama yake mjini Toronto, Kanada Februari 9, 2005.Picha: AP

Kesi hii si muhimu tu kwa mustakabali wa mshtakiwa Omar Khadr bali ina umuhimu mkubwa kwa Rais wa Marekani Barack Obama pia. Kesi hiyo dhidi ya Khadr katika mahakama ya kijeshi ni ya kwanza kusikilizwa Guantanamo tangu Obama aliposhika madaraka na kutaka kukifunga kituo hicho cha kijeshi.

Omar Khadr alikamatwa mwezi Julai mwaka 2002 katika kambi ya Al-Qaeda nchini Afghanistan. Inasemekana kuwa katika mapigano yaliyozuka kati ya wanamgambo na wanajeshi wa Kimarekani, Khadr alimrushia guruneti mwanajeshi wa Marakeni na hivyo kusababisha kifo chake. Hayo ni mashtaka makuu yanayomkabili Khadr mahakamani. Katika mahojiano na CNN, jemadari wa zamani John Altenburg alieshughulikia mahakama ya kijeshi ya Guantanamo wakati wa serikali ya George W. Bush amesema:

" Kuna ushahidi kuwa yeye ndio alierusha guruneti iliyomuuwa mwanajeshi wa Kimarekani."

Lakini hayo yamekanushwa na luteni kanali Jon Jackson anaemtetea Khadr.Yeye amesema:

" Ushahidi kuhusu tukio hilo ni dhahiri kabisa kuwa Omar Khadr hakurusha guruneti hiyo."

Khadr mwenye umri wa miaka 23 anashtakiwa pia kutengeneza miripuko na kusaidia ugaidi. Tukio la kumkamata Omar Khadr lilishtusha kwani wakati huo alikuwa na umri wa miaka 15 tu. Mtetezi Jackson anasema Khadr alikuwa askari mtoto kwa hivyo lazima ahurumiwe. Lakini mwendesha mashtaka mmojawapo ameshatamka waziwazi kuwa umri usizingatiwe wakati wa kuiendesha kesi hiyo na kuamuliwa iwapo ana hatia au la. Suala la umri lizingatiwe tu wakati wa kuamua muda wa kumfunga jela Khadr.

In this photo taken Wednesday, May 13, 2009 and reviewed by the U.S. military, the sun rises over the Guantanamo detention facility at dawn, at the Guantanamo Bay U.S. Naval Base, Cuba. In a speech Thursday, President Barack Obama defended his plans to close the Guantanamo prison camp. (AP Photo/Brennan Linsley
Jela ya jeshi la Marekani Guantanamo.Picha: AP

Jackson amemkosoa vikali Rais Obama alieahidi kukifunga kituo cha Guantanamo mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani. Yeye analaumiwa kungángánia mahakama ya kijeshi iliyoanzishwa na serikali ya Bush kwa ajili ya wafungwa wa Guantanamo. Obama ameamua kufungua ukurasa mpya kuhusu kituo hicho, lakini kwa bahati mbaya ukurasa huo unaanzia kwa kesi ya askari mtoto.

Hata hivyo, serikali ya Obama imebadili mfumo wa kazi wa mahakama hiyo ya kijeshi. Kwa mfano, haiwezekani tena kutumia ushahidi unaopatikana kwa kuwatesa washukiwa. Na Khadr anasema utaratibu huo wa mateso ulitumiwa kumlazimisha kukiri makosa alipokuwa akihojiwa. Khadr ana uraia wa Kanada kwani alizaliwa nchi hiyo na aliishi huko mpaka alipokuwa na umri wa miaka tisa, ambapo aliondoka na baba yake aliehamia Afghanistan pamoja na familia yake. Mwandishi wa habari Spencer Ackerman aliewahi kuhudhuria vikao vya kuwahoji washukiwa kabla ya kufikishwa mahakamani anasema Kanada wala haina mpango wa kumchukua Khadr kwani serikali haikutoa ombi la kurejeshewa raia wake.

Mwandishi: Ziegler, Albrecht/ZPR

Mhariri: Charo,Josephat