1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Askari wa Umoja wa Mataifa wauawa nchini Lebanon

9 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cmxz

BEIRUT:

Bomu moja ambalo lilikuwa kando ya barabara limelipuka kusini mwa Lebanon na kuwajeruhi askari wawili wa kikosi cha Umoja wa Matiafa kinacholinda amani huko.

Duru za Umoja wa Mataifa zimeeleza kuwa bomu hilo lililengwa kwa kikosi hicho UNIFIL.Mlipuko huo ndio wa tatu kutokea dhidi ya walinda usalama wa Umoja wa mataifa nchini Lebanon tangu kikosi hicho kilipoongezewa askari zaidi wanaofikia 13,000 tangu mgogoro wa Israel na kundi la wanamgambo wa Lebanon la Hezbullah mwaka wa 2006.Kikosi cha UNAFIL kiliundwa mwaka 1978 na Umoja wa Matifa ili kuhakikisha kuwa Israel imeondoa majeshi yake kutoka Lebanon na pia kurejesha amani na usalama katika eneo hilo.