1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASMARA: Waingereza waliotoweka Ethiopia waendelea kusakwa

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMH

Eritrea imekanusha kuhusika kwa njia yo yote ile na kutoweka kwa kundi la Waingereza,ikidhaniwa kuwa wametekwa nyara.Msemaji wa serikali ya Eritrea amesema,lawama kuwa imehusika na tukio hilo,hazina msingi wo wote.Waingereza 5,ikiwa ni pamoja na wafanya kazi wa ubalozi wa Uingereza mjini Addis Ababa na pia Waethiopia 13,walitoweka siku ya Alkhamisi,katika eneo la Afar,kaskazini-mashariki ya Ethiopia.Ripoti zinasema,Waethiopia 5 kutoka kundi hilo wamegunduliwa na wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wakipiga doria karibu na mpaka wa Eritrea.Wakati huo huo tume ya maafisa kutoka wizara ya nje ya Uingereza imewasili mji mkuu wa Ethiopia,Addis Ababa,ikisemekana kuwa wanajeshi wa Kingereza wa tabaka ya juu wamekaa tayari.