1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

"Assad astahili kufunguliwa mashtaka," Waziri wa Ufaransa

23 Mei 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa amesema leo kuwa Rais wa Syria Bashar al-Assad anapaswa kufunguliwa mashtaka.

https://p.dw.com/p/4RhQ2
Syrien Machthaber Assad tritt vierte Amtszeit an
Picha: SYRIAN PRESIDENCY FACEBOOK PAGE/AFP

Kufuatia "mamia kwa maelfu ya vifo" na "matumizi ya silaha za kemikali" wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Catherine Colonna amesema vita dhidi ya uhalifu na kupinga ukwepaji wa mkono wa sheria ni sehemu ya sera za diplomasia ya Ufaransa. Hata hivyo Colonna amesema serikali ya Paris haitobadili sera yake kuelekea mtawala waSyria na kusema kuwa Assad amekuwa adui wa watu wake kwa zaidi ya miaka 10.

Soma pia: Assad wa Syria kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Kiarabu

Bashar al Assad amerejea katika jukwaa la siasa za kikanda baada ya taifa lake kukaribishwa ten ndani ya Jumuiya ya nchi za Kiarabu baada ya kutengwa kwa muongo mmoja.