1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Assange amtaka Obama akome kuifuatilia WikiLeaks

Josephat Nyiro Charo19 Agosti 2012

Muasisi wa tovuti ya WikiLeaks, Julian Assange, ameyasema hayo leo (19.08.2012) alipotoa hotuba akiwa kwenye roshani ya ubalozi wa Ecuador mjini London, Uingereza, miezi miwili tangu alipojificha katika ubalozi huo.

https://p.dw.com/p/15sh9
WikiLeaks founder Julian Assange gives a thumbs up sign after speaking to the media outside the Ecuador embassy in west London August 19, 2012. Assange used the balcony of Ecuador's London embassy on Sunday to berate the United States for threatening freedom of expression and called on U.S. President Barack Obama to end what he called a witch-hunt against WikiLeaks. REUTERS/Olivia Harris (BRITAIN - Tags: POLITICS CRIME LAW MEDIA)
Wikileaks Gründer Julian Assange Aufenthalt Botschaft Ecuador in LondonPicha: REUTERS

Muazilishi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange amemtaka rais wa Marekani, Barack Obama, kusitisha ufuatiliaji wa maonevu dhidi ya mtandao huo. Assange amesema huku mtandao wa WikiLeaks ukikabiliwa na kitisho, ndivyo uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa jamii zetu unavyokabiliwa pia na kitihso hicho.

"Tunalazimika kutumia fursa hii kueleza kwa ufasaha chaguo lililo mbele ya serikali ya Marekani. Je, Marekani itarudi na kusititiza maadili ya mapinduzi yaliyotumiwa kuliunda taifa hilo? Au itatuvuruta sote katika ulimwengu hatari kandamizi, ambamo waandishi wa habari wananyamaza kimya kwa hofu ya kushitakiwa na walimwengu wanalazimika kunong'nezana gizani?" Assange ameitaka Marekani isichukue mkondo huo na kuitolea mwito ikomeshe vita vyake dhidi ya watu wanaofichua siri.

"Namtaka rais Obama afanye kitu kilicho sahihi, Marekani lazima iachane na uchunguzi wake dhidi ya mtandao wa WikiLeaks," amesema Assange alipotoa tamko lake la kwanza hadharani tangu Ecuador ilipompa ukimbizi wa kisiasa Alhamisi iliyopita.

Assange aipongeza Ecuador

Assange ameupongeza ushujaa ulioonyeshwa na rais wa nchi hiyo ya Amerika ya Kusini, Rafael Correa. "Namshukuru rais Correa kwa ushujaa aliouonyesha katika kuzingatia ombi langu na kunipa ukimbizi wa kisiasa," alisema Assange wakati alipozungumza na vyombo vya habari vya kimataifa vilivyokuwa vimekusanyika nje ya ubalozi wa Ecuador jijini London.

Ecuadorian President, Rafael Correa, waves at his arrival to the National Court of Justice of Ecuador in Quito, on 24 January 2012. Correa described the suspension of the hearing today, due the illness of one of the three judges in charge of the process against El Universo newspaper for a column that the president considered offensive as a "new trick", and Correa accused the newspaper of wanting to discredit the new National Court of Justice. EPA/Jose Jacome +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais wa Ecuador, Rafael CorreaPicha: picture-alliance/dpa

Assange amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza tangu alipojificha katika ubalozi wa Ecauador nchini Uingereza miezi miwili iliyopita. Kujitokeza katika roshani ya ubalozi huo kumeonekana kama jitihada ya kukwepa kukamatwa. Raia huyo wa Australia anatakikana na Sweden kuhojiwa kuhusu madai ya unyanyasaji wa ngono.

Assange awashukuru wafuasi wake

Muasisi huyo wa mtandao wa WikiLeaks pia aliwashukuru wafuasi wake. Kwa watu wa Marekani, Uingereza, Sweden na Australia walioniunga mkono licha ya serikali zao kutofanya hivyo, na kwa maafisa wenye busara wa serikali za nchi hizo, ambao wanaendelea kupigania haki, siku yenu inakuja," amesema Assange.

Amewashukuru wafanyakazi na wafuasi wa Wikileaks ambao uhodari wao na kujitolea kwao kusiko kifani. Ameiambia familia yake na watoto wake ambao amesema wamenyimwa baba yao, kwamba wataungana tena hivi karibuni.

Assange ataka Bradley Manning aachiwe huru

Mtandao wa WikiLeaks ulichapisha maelfu ya nyaraka za siri za kidiplomasia za Marekani mnamo mwaka 2010. Mtaalamu wa kijasusi wa jeshi la Marekani, Bradley Manning, anayeshutumiwa kwa kufichua taarifa hizo anazuiliwa katika kambi ya kijeshi ya Marekani. Assange ametaka Manning aachiwe huru.

Army Pfc. Bradley Manning is escorted by military police from the courthouse after the sixth day of his Article 32 hearing at Fort Meade, Maryland in this December 21, 2011 file photo. Manning, the U.S. Army intelligence analyst suspected of passing classified documents to WikiLeaks, will face a full court-martial, the U.S. Army Military District of Washington announced on February 3, 2012. REUTERS/Benjamin Myers/Files (UNITED STATES - Tags: CRIME LAW MILITARY HEADSHOT)
Bradley ManningPicha: REUTERS

"Kama Bradley Manning alifanya kama anavyoshutumiwa basi yeye ni shujaa na mfano kwetu sote na mmoja wa wafungwa wa kisiasa duniani. Bradley Manning lazima aachiwe."

Assange amesema Manning alikamilisha siku yake ya 815 ya kuzuiliwa bila kufunguliwa mashitaka. Kisheria mtu anatakiwa kuzuiliwa bila kufunguliwa mashitaka kwa siku 120.

Assange azungumzia kuhusu bendi ya Pussy Riot

Assange amezungumzia pia hukumu ya miaka miwili jela dhidi ya wanachama wa bendi ya Pussy Riot nchini Urusi. Bendi hiyo ilitiwa hatiani kwa makosa ya uhaini na uchohezi wa kidini kwa kuimba wimbo unaomkpionga rais Vladimir Putin katika kanisa moja la mjini Moscow mapema mwaka huu.

Die drei Mitglieder der kremlkritischen Punkband Pussy Riot sitzen am 17.08.2012 in einem Glaskäfig in einem Gericht in Moskau: (l-r) Maria Aljochina, Jekaterina Samuzewitsch und Nadeschda Tolokonnikowa. Die Mitglieder der Band Pussy Riot müssen nach ihrem Protest gegen Kremlchef Putin in einer Kirche für je zwei Jahre in Haft. Richterin Marina Syrowa begründete das Strafmaß am Freitag mit Rowdytum aus religiösem Hass. Die Untersuchungshaft von knapp sechs Monaten werde angerechnet. Foto: Andrey Stenin/RIA Novosti
Wanachama wa bendi ya Pussy RiotPicha: picture-alliance/dpa

Assange pia amezungumzia hukumu ya miaka mitatu gerezani iliyotolewa na mahakama moja ya Bahrain dhidi ya rafiki yake, Nabil Rajab, Alhamisi iliyopita. Nabil, ambaye ni mkuu wa tasisi ya kutetea haki za binaadamu nchini Bahrain, alihukumiwa kwa kuongoza maandamano dhidi ya utawala wa nchi hiyo mnamo mwezi Machi mwaka jana. Amekuwa akizuiliwa tangu Juni mwaka huu kwa kuitusi jamii ya Wasunni nchini Bahrain kupitia tovuti ya kijamii ya twitter.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Iddi Sessanga