1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASTANA: Chama tawala kinadhibiti bunge Kazakhstan

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXo

Kwa mujibu wa matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa bunge uliofanywa nchini Kazakhstan siku ya Jumamosi,chama tawala cha Rais Nursultan Nazarbayev kimeimarisha wingi wake bungeni.

Matokeo ya mwanzo yanaonyesha kuwa chama tawala „Nur Otan“ kimejinyakulia asilimia 88 ya kura zilizopigwa na kitadhibiti viti vyote bungeni.Ikiwa matokeo ya mwanzo yatabakia kama hivi sasa,basi vyama vingine vitashindwa kuvuka kiwango cha asilimia 7 kinachohitajiwa ili kuweza kuingia bungeni.