1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASUNCION: Rais Köhler-utandawazi usaidie wamasikini

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCM0

Rais Horst Köhler wa Ujerumani,amewasili nchini Paraguay akiwa katika ziara ya siku 12 barani Amerika ya Kusini.Alipozungumza baada ya kukutana na rais mwenzake Nicanor Duarte Frutos,Rais Köhler alisema,utandawazi unapaswa kuwaruhusu watu wote kunufaika kutokana na maendeleo ya kiuchumi.Akaongezea kuwa umasikini ni sababu mojawapo kuu ya ugaidi na uhalifu.Vile vile ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa na biashara kufanyia kazi usawa wa kijamii.Rais Köhler atabakia Paraguay mpaka siku ya Jumatano.Baadae ataelekea Brazil na Colombia.