1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Atangaza ushindi

18 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIm3

KOSOVO:

Kiongozi wa zamani wa waasi wa Kosovo,Hashim Thaci amejitangaza mshindi katika uchaguzi wa jana wa bunge huko Kosovo,mkoa wa Serbia unaotawaliwa na UM.Hatima ya Kosovo bado haijulikani iwapo itakuwa huru au la.Matokeo ya awali yakionesha chama cahke cha PDK kikiongoza kwa 35% dhidi ya Democratic League cha rais Fatmir Sejdiu chenye viti 22.Uchaguzi wa jana uligubikw na ukosefu mkubwa wa wapiga kura na wakaazi wachache wa asili ya serbia waliususia.Waserbia wanawapinga waalbania walio-wengi mkoani Kosovo kujitangazia uhuru.

Desemba 10 ijayo ni tarehe ya mwisho kujua iwapo mazungumzo ya kimataifa juu ya hatima ya kosovo kukamilishwa mjini Brussels.

Mazungumzo hayo yamekwama kwa miezi kadhaa sasa.