1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Athari ya mashambulizi ya maneno mitandaoni

Mohammed Khelef
22 Novemba 2016

Licha ya uzuri uliomo kwenye mitandao ya kijamii kwa kuuwaunganisha watu na kurahisisha ufanyaji biashara na ujasiriamali miongoni mwa vijana, lakini pia kumezuka kiwango kikubwa cha matusi na kashfa kupitia mitandao hiyo, katika kile kinachoitwa Cyber Bullying, ambako katika baadhi ya matukio, wanaoelekezwa na mashambulizi hayo hukaribia hata kupoteza maisha.

https://p.dw.com/p/2T2uX

Mohammed Khelef, ambaye alikuwa kwenye ziara ya kuangalia matumizi ya mitandao ya kijamii miongoni mwa vijana wa miji ya Afrika Mashariki, alikutana na kijana Michael Otieno katika mkahawa mmoja jijini Nairobi, na wakazungumzia namna mashambulizi ya maneno kwenye mitandao ya kijamii yalivyoshamiri katika mji huo mkuu wa Kenya.