1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS: Misitu inateketea kwa moto barani Ulaya

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBes

Wimbi la joto kali Kusini-Mashariki ya bara Ulaya,limesababisha moto katika misitu ya kanda hiyo.Maelfu ya watalii,wamehamishwa kutoka maeneo ya mapumziko yanayokabiliwa na hatari ya kushika moto.Kama watu 5,000 wamekimbia uwanja wa kupiga kambi,ulioshika moto kusini mwa Italia.Hata nchini Croatia,mamia ya watalii walihamishwa, baada ya misitu kushika moto ukingoni mwa pwani ya Bahari ya Adriatiki.Ugiriki nayo,tangu majuma kadhaa inapigana na moto inayoteketeza misitu, huku wanamazingira wakiamini kuwa baadhi ya moto, imeanzishwa kwa makusudi.