ATHENS: Misitu na nyumba zateketezwa na moto
28 Julai 2007Matangazo
Wazima moto nchini Ugiriki na Italia wanaendelea kupambana na moto uliosambaa misituni.Maafisa kusini mwa Italia,wametangaza hali ya maafa baada ya misitu kuendelea kushika moto tangu siku tano, kwa mfululizo.Zaidi ya wazima moto 200 wakisaidiwa na wanajeshi na helikopta mbili wanahangaika kuzima moto ulioteketeza kiasi ya nyumba 100 katika eneo la kusini la Peloponnes. Bulgaria na Croatia pia zimeripoti juu ya misitu iliyoshika moto.