1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS: Ubalozi wa Marekani washambuliwa

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbG

Washambuliaji wamevurumisha roketi ndani ya ubalozi wa Marekani mjini Athens Ugiriki mapema leo. Jengo la ubalozi huo limeharibiwa kidogo lakini hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika hujuma hiyo. Roketi hilo lilivurumishwa kutoka upande wa pili wa barabara.

Akizungumza kuhusu shambulio afisa wa ubalozi wa Marekani mjini Athens amesema, ´Hatukutarajia lolote lakini ubalozi bila shaka hulindwa kama tunavyolinda balozi zetu nyengine ulimwenguni kote. Nalichukulia kama shambulio baya sana.´

Maofisa wa usalama wanachunguza madai kwamba kundi la mapinduzi, ´Revolutionary Struggle´ limefanya shambulio hilo. Kundi hilo limeibuka kuwa hatari kwa usalama tangu kundi lengine la waasi liitwalo ´Novemba 17´ lilipopigwa marufuku mnamo mwaka wa 2002.

Kundi la Novemba 17 lilitangaza kuhusika na mauaji ya waziri wa utamaduni wa Ugiriki mnamo mwezi Mei mwaka jana na shambulio la bomu miezi 13 iliyopita katika wizara ya uchumi, lililowajeruhi watu wawili na kuyaharibu majengo.