1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS: Wakimbizi wamezama nje ya pwani ya Ugiriki

17 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRI

Maiti za Waafrika 5 waliotaka kukimbilia Ulaya kwa njia isiyo halali zimepatikana na 20 zingine zinakosekana,baada ya boti iliyopakia wahamiaji hao,kuzama nje ya pwani ya kisiwa cha Kigiriki cha Samos.Mtu mmoja alienusurika amewaambia maafisa wa Ugiriki kuwa boti hiyo iliokuwa na Wasomali 26,ilizama mashariki ya Bahari ya Aegean karibu na pwani ya Uturuki Ijumaa jioni.Wizara ya meli za biashara ya Ugiriki imesema boti za doria,meli ya jeshi la wanamaji na helikopta zinasaka eneo hilo.Siku kumi zilizopita,si chini ya maiti 7 zilikutikana baada ya boti inayofanya safari za haramu za kusafirisha binadamu,kuzama nje ya Samos.