1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS:Chama cha New Democracy chashinda tena katika uchaguzi

17 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPA

Waziri mkuu wa Ugiriki Costas Karamanlis ameshinda tena katika uchaguzi uliofanyika baada ya kashfa ya pesa vilevile mkasa wa moto uliosababiosha vifo vya watu 65 mwezi jana.Bwana Karamanlis ameshinda muhula wa pili wa miaka minne.Wafuasi wa chama chake cha New Democracy walimiminika kwenye barabara za mji wa Athens kusherehekea ushindi huo.Taarifa yake ya kuwashukuru wapiga kura ilitolewa muda mfupi baada ya mpinzani wake mkuu George Papandreou wa chama cha kisoshalisti cha PASOK kukubali kushindwa.Matokeo yanaonyesha kuwa chama cha New Democracy kimepata asilimia 42 huku cha PASOK kikiwa na asilimia 38 ya asilimia 85 ya kura zote zilizohesabiwa.

Kulingana na matokeo hayo chama cha New Democracy kina uwezo wa kushinda viti vya kutosha bungeni ili kuunda serikali.