1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATLANTA : Gwiji wa Muziki wa Soul James Brown afariki

26 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCg6

James Brown Gwiji wa Muziki wa Mtindo wa Soul ambaye sauti yake,mtindo wake wa kucheza na mpangilio wa muziki wake umeleta mdundo wenye hisia kwenye ulimwengu wa muziki na kushawishi kizazi cha wanaumiziki weusi nchini Marekani amefariki dunia wakati wa usiku wa manane wa X’masi hapo jana akiwa na umri wa miaka 73.

Brown alifariki kutokana na msokoto wa moyo hapo sasa nane kasorobo usiku wa mkesha wa X’masi katika hospiatli ya Emory Crawford Long huko Atlanta.

Brown alikwenda kumuona daktari wa meno wiki iliopita ambaye alimuona akikohowa na kumshauri kumuona daktari ambapo alilazwa hapo Jumamosi akiwa na kichomi kikali.

Kwa mujibu wa meneja wake binafsi na rafiki wa muda mrefu Charles Bobbit gwiji huyo wa muziki alikuwa na maumivu hapo kabla lakini baadae yaliondoka na alimwambia muda mfupi kabla ya kuaga dunia kwamba alikuwa anaondoka duniani usiku huo.

Rais George W. Bush wa Marekani amesema amesikitishwa na kifo cha Gwiji huyo wa Musiki wa Soul ambaye kwa nusu karne ubunifu wa kipaji chake cha muziki huo ulitajirisha utamaduni wa Marekani na kushawishi vizazi vya wanamuziki.