1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATLANTA: Watu takriban wanane wauwawa

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNI

Watu takriban wanane wameuwawa kwenye kimbunga kilichopiga katika jimbo la Alabama nchini Marekani. Wanafunzi watano katika shule moja ya upili ni miongoni mwa waliouwawa huku wanafunzi wengine wakifunikwa chini ya paa lililoporomoka.

Ripoti za awali zilisema idadi ya waliouwawa ilikuwa watu 15 lakini maofisa wamethibitisha ni watu wasiopungua wanane waliokufa kutoka na kimbunga hicho.

Watu zaidi ya 40 walilazwa hospitalini wakati kimbunga hicho kikali kilipokuwa kikivuma katika jimbo hilo la Alabama.