1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azimio dhidi ya Syria

5 Oktoba 2011

Urusi na China ziliungana hapo jana kupinga rasimu ya mataifa ya Ulaya ya azimio la baraza la usalama la Umoja wa mataifa, linaloashiria kuwa huenda Syria ikakabiliwa na vikwazo iwapo itaendelea na ukandamizaji

https://p.dw.com/p/12ljP
Baraza la usalama la Umoja wa mataifaPicha: dapd

Azimio hilo lilipokea kura 9 za kuliunga mkono na wanachama wanne walikataa kupiga kura.

Walid Al-Moualem syrischer Außenminister vor den UN in New York
Waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid Al-MoualemPicha: AP

Urusi na China zilikuwa ni wanachama wa pekee waliopiga kura ya kupinga azimio hilo lililoandikwa na Ufaransa kwa ushirikiano na Uingereza, Ujerumani na Ureno.

Mataifa ya Ulaya yalipendekeza azimio ambalo litatishia kuchukuliwa hatua zilizolengwa iwapo rais Bashar al Assad hatositisha msako wake mkali katika muda wa siku 30.

Mwandishi Maryam Abdalla/dpa ap rtr afp