1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azimio la Umoja wa Mataifa dhidi ya adhabu ya kifo

19 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdUi

NEW YORK

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitsiha azimio lisiloloshurutisha lenye kutowa wito wa kuzuwiya kwa muda adhabu za kifo.

Azimio hilo limepitishwa kwa kura 104 dhidi ya 54 wakati wajumbe wengine 29 hawakushiriki katika kura hiyo.Italia ikizungumza kwa niaba ya Umoja wa Ulaya ni mtetezi mkuu wa azimio hilo.Marekani,Misri,Iran na nchi nyingi za Asia zimepiga kura kupinga azimio hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu Amnesty International Marekani,Pakistan na Sudan hufanya kama asilimia 90 ya hukumu za kifo zinazotolewa duniani kote.

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kuongeza muda wa mamlaka ya vikosi vinayvoongozwa na Marekani nchini Marekani kwa mwaka mmoja zaidi.