1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baada ya kuchaguliwa mwenyekiti

18 Septemba 2008

Baada ya kuchaguliwa Zipi Livni mwenyekiti wa Kadima kitafuata nini Israel ?

https://p.dw.com/p/FKog

Waziri mkuu atakemfuata huyu wa sasa anaeacha madaraka Ehud Olmert nchini Israel, pengine atakuwa mwanamke:Bibi Zipi Livni, waziri wa sasa wa mambo ya nje.Bibi Livni alishinda jana uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa chama-tawala cha Kadima.Akifanikiwa katika juhuidi zake za amani na wapalestina,hatahitaji kuhofia kushindwa ukiitishwa uchaguzi mpya.

Uchambuzi wa Peter Philipp mnasimuliwa studioni na Ramadhan Ali:

Matokeo ya uchaguzi wa chama jana yaliongoza ushindi wa chupuchupu wa Bibi Livni,lakini ulitihibitisha ilivyobashiriwa kwamba atashinda ingawa haikuwa kwa asili mia 10 au 12 bali 1 tu. Bibi Livni alijipatia kura 431 zaidi kuliko mpinzani wake waziri wa mawasiliano na uchukuzi Bw. Mofaz.Hatahivyo, zilitosha kumkabidhi dhamana ya kuanza kuunda serikali mpya ya Israel au kuifanya kazi hiyo kuwa ngumu kwake kuparamia kileleni mwa serikali ya Israel.

Na si maneno matupu usemi kwamba, Israel ndio demokrasia pekee katika Mashariki ya kati.Hatahivyo, Israel inajikuta kwa mara ya pili ikibadili kiongozi wa kisiasa bila kupitia uchaguzi.

Utakumbuka waziri mkuu Ariel Sharon aliechaguliwa na umma alipokumbwa na maradhi ya kuzimia hapo Januari 2006,hatamu za uongozi wa serikali alikabidhiwa makamo wake Ehud Olmert.Halafu vishindo alivyotiwa vilipomzidi kutokana na tuhuma za kula rushua,chama cha Kadima kikaanda uchaguzi wa kupata mwenyekiti mpya.Wapigakura 74.000 wa chama wakabidi kuamua Israel iendelee vipi.Ni kiasi cha nusu ya wapiga kura hao-55% ndio waliokwenda jana kupiga kura.

Hii ikawa sababu ya kutosha kwa mshirika serikalini chama cha Leba kikiongozwa na waziri wa ulinzi Ehud Barak,tena masaa tu baada ya kujulikana matokeo kilidai kuitishwa uchaguzi mpya nchini kote Israel.Kilidai umma uamue na umma utaamua kufuata mkondo wa chama cha Leba.

Ikiwa kutaitishwa uchaguzi mpya nchini Israel,mapema kabisa utafanyika mwezi Machi mwakani.Na hadi wakati huo, Israel itajikuta katika kampeni ya uchaguzi.Hiyo ni hali ambayo italemaza shughuli zote.Na hasa juhudi za amani zilizoanza kutoa sura za kuleta mapatano na wapalestina-juhudi ambazo zilikwishazorota zikisubiri kutawazwa kwa rais mpya nchini Marekani.

Halafu sasa kimeibuka chama cha Leba chenye ndoto ya kushinda uchaguzi mpya.Inaonekana sana hali ikawa vyengine kabisa. Chama cha bw.Barak kitabakia dhaifu na hata chama cha Kadima kitadhofika . Upande wa tatu utakaonufaika huenda ikawa ule wa waziri mkuu wa zamani Bednjamin Netanyahu ambae alisalia katika chama cha Likud baada ya mpasuko uliozaa Kadima.

Hii itakua na maana gani,haimbidi mtu kuchunguza sana.Alikuwa Natanyahu alieyavuruga mapatano ya Oslo na kuyaangusha.Juhudi za amani si jambo linalotanguliwa usoni kabisa katika siasa za Israel,lakini pia bila juhudi hizo hakuna kinachoenda.Ndio sababu yampasa mtu kubakia na matumaini Bibi Livni anasonga mbele na majadiliano na wapalestina hadi kuyafanikisha.

Akifanikiwa,basi hataku