1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baada ya uchaguzi Zambia

4 Novemba 2008

Kiongozi wa Upinzani M.Sata hautambui ushindi wa rais Banda nchini Zambia.

https://p.dw.com/p/FnEa

Kufuatia uchaguzi wa Zambia na kutawazwa haraka-haraka kwa rais Rupiah Banda, juzi jumapili,kiongozi wa Upinzani Michael Sata, kwa mara ya nyengine leo, amekataa kuutambua ushindi wa Rupiah Banda katika uchaguzi wa wiki iliopita wa urais wa Zambia.

Hatua yake hii, imefungua mlango wa mabishano marefu ya kisiasa katika nchi hii ya kusini mwa Afrika, jirani na Zimbabwe iliotumbukia pia katika mvutano wa aina hiyo.

„Sikushindwa uchaguzi huu" alinukuliwa Kiongozi huyo wa Upinzani mwenye umri wa miaka 71 kuiambia Radio ya Afrika kusini (SAfm) „.

Sata akaongeza kusema na ninamnukulu tena,

„Rupiah Banda hana upeo. Banda hana jukwaa la kisiasa.Jukwaa pekee la Banda ni kudanganya."

Chama cha Patriotic Front cha Bw.Sata kilipanga kwenda Mahkamani hii leo kupinga ushindi wa chupouchupu aliopewa Banda dhidi ya kiongozi wa chama hicho Michael Sita aliekuwa akiongoza awali katika matokeo ya uchaguzi huo wa rais.

Rupiah Banda, pia akiwa na umri wa miaka 71 aliapishwa jumapili papara-papara Kujaza pengo la kiti cha rai wa Zambia kilichoachwa wazi na kifo cha rais Levy Mwanawasa.Mwanawasa alifariki dunia hapo August baada ya kupigwa na maradhi ya kiharusi.

Tume ya Uchaguzi ya Zambia ilitangaza kwamba ,mjumbe huyo wa zamani wa kibalozi Banda alijipatia 40.9% ya kura dhidi ya 38.13% za mpinzani wake Michael Sata. Sata amebae alishindwa pia uchaguzi wa Rais mara 2 kwanza 2001 na tena 2006 na marehemu Mwanawasa,anatuhumu kwamba uchaguzi ulipitishiwa mizengwe na kudai miongoni mwa mambo mengine upigaji kura ukiendelea sememu nyengine wakati matokeo ya kwanza yakitolewa.Timu mbili za wachunguzi za kiafrika lakini ziliueleza uchaguzi hu ukuwa ulipita bila ya hitilafu.

Jeshi na vikosi vya polisi vya Zambia vimekuwa macho tangu Wiki iliopita Kuzuia fujo lolote litakalozuka baada ya uchaguzi.Machafuko kidogoi tu yalizuka katika sememu za mji mkuu Lusaka na katika jimbo la machimbo ya shaba kwa muujibu wa taarifa za mwishoni mwa Wiki.

Katika uchaguzi uliopita wa 2006 pale kiongozi wa upinzani Michael Sata alipokataa kuutambua ushindi wa Mwanawasa kulizuka fujo kubwa na hasa mji mkuu Lusaka.

Zambia, mzalishaji mkubwa wa madini ya shaba barani Afryka,65% ya wakaazi wake milioni 11 wanaishi si kwa zaidi ya dala 1 kwa siku.Banda ameahidi kuendeleza sera za kiuchumi za rais aliemtangulia Levy Mwanawasa zilizovutia nchini watiaji raslimali wa kigeni na hata wafadhili.