1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baada ya ziara ya Bush Mashariki ya kati

17 Januari 2008

Matokeo ya ziara ya siku 8 ya George Bush Mashariki ya kati ni haba.Hakuna kikubwa kilichofanikiwa.

https://p.dw.com/p/Ct9Y
George W. Bush na rais MubarakPicha: AP

Ziara ya wiki moja ya rais George Bush wa Marekani huko Mashariki ya kati ilimalizika jana nchini Misri,kituo chake cha mwisho.Azma ya Bush ilikua kuusukuma mbele Utaratibu wa amani wa Mashariki ya kati .Lakini, rais huyu anaeondoka madarakani karibu ni,hakujenga msingi barabara wa utaratibu huo na hivyo, si mengi aliyojipatia anasema mchambuzi wetu wa maswali ya Mashariki ya

George Bush aliazimia kufanya mengi katika safari yake hiyo ya siku 8 na akiwa pekee na kuwaza ataungama kwamba shabaha aliolenga kuifikia hata hajainyemelea.

Bush alitaka kusukuma mbele juhudi za amani baina ya waisraeli na wapalestina , alitaka kuikuza na kuimarisha safu ya vita dhidi ya Iran , alitaka kupalilia zaidi na kustawisha demokrasia katika Ghuba au Mashariki ya kati na hata kushawishi kuteremshwa kwa bei ya mafuta ya petroli.

Hakuna chochote kati ya hayo yote aliobainika George Bush amefaulu.

Kwahivyo, matarajio yalionigin'nizwa juu ya safari yake yafaa kuzikwa.Bush alitaka kutokana na mafanikio yake Mashariki ya kati kujiandikia sahifa katika historia kuwa amefanya mema wakati wa wadhifa wake.

Shinani kabisa katika ziara hii ilikua kitandawili kati ya waisraeli na wapalestina na jinsi ya kukifumbua.Ni yeye lakini aliekiachia kitandawili hicho kwa miaka 7 bila kujaribu kukifumbua na sasa ni wazi kabisa kile ambacho hajakipanda hawezi sasa kukivuna.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais Mahmud Abbas wa Palestina ili wabaki hayi kisiasa wana hamu kubwa ya kuona wanafanikiwa na hivyo ni wazi wanabidi kushirikiana nae na kuwa tayari kuzungumzia hata maswali nyeti na ya kimsingi ya mzozo huu.

Kwa utayarufu huop,Olmert ameshapoteza mshirika mmoja katika serikali yake ya muungano ya mrengo wa kulia nchini Israel.Hadi sasa lakini, hakuyaondoa maskani yoyote yale ya wayahudi yaliojengwa kinyume na sheria ,hakuondosha pingamizi zozote majiani vinayozuwia nyendo za wakaazi wa kipalestina na badala ya kufanya hivyo, Olmert ametia kasi na kuimarisha vita dhidi ya Hammas katika mwambao wa gaza na hata katika ukingo wa magharibi.

Kuregeza kidogo zaidi kamba sio tu kungemsaidia Mahmud Abbas bali hata pia mazungumzo ya George Bush aliofanya katika Ghuba tangu mjini Riadh lakini hata Sham el Sheikh, nchini Misri.

Nchi hizo 2 zitayari kuungamkono amani baina ya Israel na wapalestina na jumuiya ya nchi za kiarabu kitambo kabisa imeeleza hayo .Wanasubiri Israel iiitikie kwa kuachana kuzin'gan'gania ardhi za waarabu na walichosikia si zaidi ya maneno matamu kutoka Washington.

Kwa kadiri Israel haikuitikia hodi za warabu,Bush asitumae waarabu wataitikia changamoto alioitoa dhidi ya Iran.Na hasa kwa kuwa hata Idara za ujasusi za marekani zimeungama kwamba Iran haina mradi wa kuunda silaha za atomiki.Waarabu katika Ghuba wanataka utulivu wao na kabisa hawataki kumpunga shetani wa Iran na kujiachia kutoswa katika balaa ambalo matokeo yake hawajui mwishoe yatakuaje.

Kuhusu kilio cha kupalilia demokrasi huko Mashariki ya kati,hakuna hata nchi moja iliovutiwa na upatu alioupiga George Bush.Kwanza ni kwa kutokana na haja ya kun'gan'gania viongozi mamlaka na pili jaribio la marekani la kuleta demokrasi Mashariki ya kati halikumvutia yeyote kuliamini.

Angalia Iraq.