1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba Mtakatifu atoa mwito Askofu Mkuu aachiliwe huru

1 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DGN8

VATIKAN:

Baba Mtakatifu Benedikt XVI ametoa mwito wa kumuachilia huru Askofu Mkuu wa Kikatoliki alietekwa nyara siku ya Ijumaa,katika mji wa Mosul kaskazini mwa Irak. Askofu Mkuu Paulos-Faraj Rahhu alikamatwa na watu waliobeba silaha,alipokuwa akitoka kanisani baada ya kusoma misa.Walinzi wake 2 na dereva waliuawa.Vikosi vya usalama vilivyosambazwa sehemu mbali mbali mjini Mosul,vinaendelea kumsaka Askofu Mkuu Rahhu.

Idadi fulani ya viongozi wa kidini wa kikristo wametekwa nyara nchini Irak,tangu nchi hiyo kuvamiwa na majeshi ya kigeni,chini ya uongozi wa Marekani katika mwaka 2003.