1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba Mtakatifu Benedict wa 16.

Mtullya, Abdu Said26 Oktoba 2008

Baba Mtakatifu Benedict wa 16 amesema atafanya ziara barani Afrika mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/Fh6C
Baba Mtakatifu Benedict wa 16 kufanya ziara barani Afrika mwaka ujao.Picha: AP

Vatican City.

Baba Mtakatifu Benedict wa 16 atazitembelea Cemeroon na Angola katika ziara yake ya kwanza barani Afrika tokea awe mkuu wa kanisa katoliki mwaka 2005

Baba Mtakatifu amesema akiwa nchini Cameroon atawasilisha matokeo ya mkutano wa baraza la maaskofu uliojadili Afrika na nchini Angola atashiriki katika maadhimisho ya miaka 500 ya injili nchini humo.