1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba mtakatifu Benedict wa kumi na sita ayatembelea maeneo takatifu nchini Israel.

Jason Nyakundi12 Mei 2009

Papa Benedict awakasirisha viongozi wa kiyahudi kutokana na matamshi yake kuhusu maangamizi ya wayahudi.

https://p.dw.com/p/HoRr
Papa Benedict katika eneo takatifu la kiyahudi nchini Israel.Picha: AP

Papa Benedict wa kumi na sita hii leo ameyatembelea maeneo matakatifu katika mji wa Jerusalem, nchini Israel, wakati ambapo kuna mzozo mkubwa kati ya Israel na Palestina, ziara ambayo pia inakabiliwa na shutuma kutoka kwa Wayahudi kutokana na aliyoyasema Papa Benedict kuhusiana na mauaji ya Wayahudi.

Papa Benedict, ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani, alisimama kwa maombi kwa dakika chache kwenye jengo la kanisa la Kirumi ambalo ni eneo takatifu zaidi baada ya kukutana na kiongozi wa Kiislamu wa Kipalestina.

Papa Benedict aliandika ujumbe wa maombi katika ukuta wa eneo hilo takatifu kabla ya kukutana na viongozi wakuu wa dini ya kiyahudi.

Ujumbe huo ulisema, nawatumia amani katika nchi hi takatifu na pia katika mashariki ya kati na katika familia yote ya wanadamu.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha radio, spika wa bunge la Israel, Reuven Rivlin, alimkemea Papa Benedict kutokana na matamshi yake ya jana jumatatu kuhusu Wayahudi milioni sita waliouawa na utawala wa Manazi.

Alikuja akatuambia kama yeye angekuwa mwanahistoria, kuhusu vitu ambavyo havingefanyika, alisema Rivlin. Katika eneo la makumbusho la Yad Vashem hapo jana, Papa Benedict alizungumzia kuhusu maangamazi ya Wayahudi, lakini aliwakasirisha baadhi ya viongozi wa Kiyahudi waliosema kuwa angeomba msamaha, kama Ujerumani na kama mkristo, kutokana na maangamizi hayo.

Papa Benedict alikuwa kijana mdogo na mwanachama wa kundi la vijana wa Hitler wakati kujiunga na kikundi hicho ilikuwa ni lazima.

Papst Benedikt mit Rabbinern in Israel an der Holocaust Gedenkstätte Jad Vashem
Papa Benedict na viongozi nchini Israel.Picha: AP

Wakati huu wa siku ya pili ya ziara yake Mashariki ya Kati, Papa Benedict alilitembelea eneo takatifu la Waislamu ambapo waumini wa dini ya kiislamu waanamini kuwa mtume Muhammad alipaa kwenda mbinguni kutoka hapo.

Kama ishara ya kuonyesha heshima, Papa alivua viatu vyake kabla ya kuingia msikitini ambao aliondoka kwenda kukutana na kiongozi wa dini ya kiislamu mjini Jerusalem.

Baadaye papa Benedict atafanya maombi katika eneo ambapo Yesu alikula chakula cha mwisho cha jioni na wanafunzi wake kabla kusulubiwa, ishara kuu ya dini ya kikiristo mjini Jerusalem, kabla ya kuendesha ibada kwa maelfu ya waumini katika shamba la Getsemane.

Papa Benedict anaitembelea Israel baada ya ziara yake nchini Jordan katika juhudi ya kumaliza tofauti kati ya Wayahudi na Waislamu, siku moja baada ya matamshi makali yaliyotolewa na kiongozi wa dini ya kiislaamu na kuyaghadhabisha makao makuu ya Vatikani na Israel.

Sheikh Taiseer al Tamimi, anayesimamia mahakama za kiislamu, alichukua kipaza sauti baada ya Papa Benedict kumaliza kuzungumza na kusema kuwa ni lazima Wakristo pamoja na waislamu waungane dhidi ya Israel.

Msemaji wa Vatikani, Federico Lombadi, aliyashtumu vikali matamshi hayo.

Mwandishi Jason Nyakundi/RTR

Mhariri Othman Miraji