1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Badiliko la hali ya hewa katika Baraza la Usalama

18 Aprili 2007

Kwa mara ya kwanza jana, Baraza la Usalama la UM lilijishughulisha na badiliko la hali ya hewa duniani.Kwani kinyan'ganyiro cha ardhi yenye rutba na maji ni ishara za hatari ya vita siku zijazo .

https://p.dw.com/p/CHG1
Ukame kaskazini mwa Kenya
Ukame kaskazini mwa KenyaPicha: DW /Maya Dreyer

Waziri wa nje wa Uingereza Margaret Becket ambae ndie aliekuwa mwenyekiti aliomnya jamii ya kimataifa juu ya athari za misiba mikubwa kutokana na badiliko hilo la hali ya hewa.

Kila kukicha joto linazidi,milima ya theluji inayayuka na maji ya baharini yanazidi kupanda na kufunika ardhi.Kwa nchi nyingi hatahivyo, athari hizo mbaya zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa zinaona ni hekaya tu ya abunuwasi.Eti si kweli.

Kwa visiwa vidogo katika bahari ya Hindi vya Maldievs hali hii maana yake ni kuvipitishia hukumu ya kifo.Kwani, vitatoweka kabisa.

“Endapo upeo wa bahari ukipanda kwa kima cha mita 2 wastani,visiwa vya Maldieve vitazama baharini.Na huo utakua mwisho wa taifa lao.”

Aliwaambia waziri wa mambo ya nje wa Maldieve Abdulla Shahid mawaziori wenzake katika Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hiyo jana .Vita vya kufa-kupona kunyan’ganyia raslimali ya maji na ardhi zav rutba siku zinazotukabili vitakua chanzo cha mabalaa mengi.

Hii ni sababu nzuri kwanini sasa Baraza la Usalama la UM kwa mara ya kwsanza jana limeanza kushughulikia athari za badiliko la hali ya hewa katika sayari yetu-kwa muujibu alivyosema waziri wa nje wa Uingereza Margaret Beckett:

“Badiliko la hali ya hewa linahatarisha amani duniani na kwahivyo, linapaswa kuwa katika ajenda ya Baraza la usalama la UM.Kuwa nchi 52 zinashiriki katika mjadala huu,ni ishara kuwa Uingereza haihisi hivyo peke yake .”

Jibu kutoka kwa kambi ya wajumbe wa urusi na china halikukawia:

Mada badiliko la hali ya hewa haihusiki kabisa kuzungumzwa katika Baraza la Usalama la UM –walidai wajumbe wan chi hizo mbili katika baraza hilo.Mjumbe wa Urusi aliomba kutotia chumvi mno .

Mbali na hayo,alisema kuna majukwaa mengine na mashirika mengine ya kuzungumzia swali hilo la badiliko la hali ya hewa.

Nae katibu mkuu wa UM Ban Ki-Moon alisisitiza na kuwazindua wajumbe kwamba hata baraza la Usalama lina jukumu la kuzungumzia swali hili.

Alisema na ninamnukulu,

“Baraza la Usalama lina linaweza hapa kutoa mchango wake kwa kushirikiana na mashirika mengine kukabili mizozo iliozuka kutokana na kuzidi kwa ujoto duniani.”

Nae waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani Bibi Heidemarie Wieczrek-Zeule akasema:

4.O-Ton Wiezoreck-Zeul engl.

“Hakuna nchi iwezayo kulitatua pekee tatizo la ukubwa huu.”

Ushirikiano wa pamoja ndio unatakikkana sasa kulikabili tatizo hili la badiliko la hali ya hewa.Maamuzi ya masilahi ya kiuchumi nay a kuvuna fedha yanayopitishwa na nchi moja yaweza kuzidhuru nchi nyengine na kuongoza katika vita.

Katika kikao cha jana cha Baraza la Usalama juu ya mada hii ya badiliko la hali ya hewa, hakuna azimio lililopitishwa na hii hakua dhamiri ya kikao hiki, alisisitiza mjumbe wa Ujerumani katika UM Bw.Thomas Matussek.