1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock aanza ziara ya wiki nzima eneo la Indo-Pasifiki

Amina Mjahid
1 Mei 2024

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameanza ziara ya wiki nzima nchini Australia, New Zealand na Fiji.

https://p.dw.com/p/4fOvi
Waziri wa mamabo ya nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock
Waziri wa mamabo ya nje wa Ujerumani, Annalena BaerbockPicha: Kira Hofmann/AA/photothek.de/picture alliance

Eneo la indo pasifiki zilipo nchi hizo tatu linaendelea kuwa muhimu kwa Ujerumani kwa sababu za kimkakati na kiuchumi. Baerbock alitarajiwa kutembelea nchi hizo mwezi Agosti mwaka jana  lakini akasitisha safari yake baada ya kutua Dubai wakati ndege ya serikali aliyokuwa anasafiria kupata matatizo ya kiufundi.

Ziara yake itaanzia Adelaide, Australia hii leo Jumatano, kisha mjini Auckland New Zealand siku ya Ijumaa kabla ya kuelekea Fiji siku ya Jumapili. Fiji iliyo na idadi ya watu chini ya milioni 1 ni moja ya nchi zinazoathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi. Watu katika baadhi ya visiwa huko wamehamishwa kufuatia mafuriko yanayosababishwa na kupanda kwa viwango vya bahari.