1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bafana bafana iko njiani kuaga Kombe la dunia na mapema ?

17 Juni 2010

Leo Nigeria na Ugiriki-nani atatamba ?

https://p.dw.com/p/Nt1Q
Vuvuzela-zazimwa jana na wauru.Je, bafana bafana buraini ?Picha: CC/Coca-Cola South Africa

Baada ya mazumari ya Vuvuzuela kunyamazishwa jana na wauru kwa kuwachapa viboko 3 Bafana bafana,leo hatima ya timu nyengine ya Afrika katika kombe hili la dunia, itaamuliwa: Nigeria yenye miadi na Ugiriki, mjini Bloemfontein, inarudi uwanjani kwa mpambano wake wapili . Wauruguay, waliowanyoa Bafana Bafana jana bila ya maji,wanasema hawafichi siri:Leo wanailalia-dago Mexico itambe mbele ya makamo-bingwa wa dunia-Ufaransa,uwanjani Polokwane. Ufaransa kama Nigeria na Ugirik, lazima zishinde leo ikiwa zisifuate nyayo za Afrika Kusini kutoa buriani kwa Kombe la Dunia 2010 .

ARGENTINA NA KOREA KUSINI:

Kabla Nigeria na Ugiriki na Ufaransa na Mexico,kuteremka uwanjani , itakuwa zamu hivi punde ya Argentina,ikiongozwa na kocha Diego Maradona, kuchuana na Korea ya Kusini.

Kocha Maradona, anabidi kucheza leo bila ya Veron,alieumia,lakini anadai anae Lionel Messi,anaeamini ndie stadi mkubwa katika Kombe hili la dunia kati ya mastadi wote.

Hatahivyo, katika mpambano wa kwa nza na Nigeria, Messi, hakufua dafu na je, leo dhidi ya Korea ya Kusini? Vipi wakorea wanacheza na timu kubwa kama Argentina, Korea ya Kaskazini nduguye,Korea ya Kusini, aliwapa salamu waargentina.Je, wakorea kusini nao watakomea lango lao kwa tumbuu la chuma ? Na, je, Gauchos-waargentina, wataweza mwishoe, kuvunja tumbuu na kuingia ndani mwa lango la Korea ya Kusini ? Majibu tutayapata kabla Nigeria kuingia uwanjani na Ugiriki.

NIOGERIA NA UGIRIKI:

Wakati kocha mashuhuri wa Ujerumani Ottmar Hitzfeld,alifaulu na timu yake ya Uswisi, jana kuwapiga kumbo magombe-dume (Torrero) ,mabingwa wa ulaya :Spain, kocha mwengine wa kijerumani, Otto Rehagel, anaeiongoza Ugiriki,atazamia nae kuwafungisha virago wanigeria na kuwafuata ndugu zao Bafana bafana nje ya Kombe la Dunia. Tangu Ugiriki hata Nigeria, kila mmoja inaelewa kwamba, leo ni kufa-kupona.Zote mbili zilishindwa mpambano wa kwanza.Nigeria na Argentina wakati Ugiriki na Korea ya Kusini.

Ikiwa leo usiku Mexico, itatamba mbele ya makamo-bingwa wa dunia-Ufaransa, timu mbili za Amerika kusini, zitaifuata Brazil duru ijayo:Kwani, zitajua kuwa, zitahitaji sare tu kwa mpambano wao wa mwisho .

Mabao 2 ya Diego Forlan, yalitosha jana kuwapiga viboko 3:0 wenyeji Bafana Bafana na kuwaandikia historia mbaya ya uwezekano wa kuwa wenyeji wa kwanza wa kombe la dunia kuaga duru ya kwanza .Bao la pili la penalty,alilotia Forlan,lilikuwa la kutatanisha,adai kocha Carlos Parraira wa Afrika kusini na anamlaumu rifu,kuliizamisha jahazi lake.

PARREIRA AMLAUMU RIFU:

Parreira, amemshambulia rifu Massimo Busacca kutoka Uswisi, kuibakisha timu yake jana na wachezaji 10 tu kwa kumuadhibu kipa wake Itumeleng Khune, kwa kadi nyekundu.Hii ni kadi nyekundu ya pili tu kuwahi kupewa kipa katika historia ya Kombe la dunia.

Parreira, alidai ," rifu wa jana, ndie mbovu kabisa hadi sasa katika kombe hili la dunia."

Ameshukuru kuwa, hatachezesha tena mechi na Afrika Kusini,alao katika Kombe hili la dunia.

Mwandishi: RamadhanAli /AFPE

Mhariri:Abdul-Rahman