BAGDAD:Desemba mwezi mbya kabisa kwa vikosi vya Marekani Iraq
31 Desemba 2006Matangazo
Jeshi la Marekani nchini Iraq limearifu kuuwawa kwa wanajeshi wake sita ndani na nje ya mji wa Baghdad na kuifanya idadi ya waliouwawa mwezi huu wa Desemba kufikia 109.
Idadi hiyo imepita ile ya mwezi wa Novemba.
Kwa jumla wanajeshi 2998 wa Marekani wameuwawa nchini Iraq tangu walipovamia mwaka 2003.Rais Gorge Bush anatarajiwa kutangaza mkakati wake mpya juu ya Iraq mwaka ujao unaoanza kesho.