1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHADAD:Umwagikaji damu waendelea Iraq

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCv1

Takriban watu 17 wameuwawa na wengine 20 wamejeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kujiripua ndani ya mkahawa katika mji mkuu wa Iraq Baghdad.

Duru za usalama za Iraq zinasema tukio hilo limefanyika kaskazini mwa Greyaat kunakokaliwa na idadi kubwa ya washia.

Wakati huo huo katika eneo la wasunni huko Baghdad kiasi watu 5 wameuwawa na wengine 25 kujeruhiwa kufuatia shambulio la kombora.