1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Abiria saba wauwawa mjini Baquba.

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzr

Nchini Iraq kundi la watu wenye silaha limeshambulia basi dogo na kuuwa abiria saba waliokuwamo ndani ya basi hilo. Basi hilo lilikuwa linaelekea katika mji mkuu Baghdad wakati lilipovamiwa kwa ghafla karibu na mji wa Baquba.

Inafikiriwa kuwa watu waliouwawa ni wa madhehebu ya Shia.

Wakati huo huo , magharibi ya Baghdad, bomu lililotegwa kando ya babarara , limesababisha wanajeshi watatu Iraq kuuwawa ambao walikuwa wakifanya doria katika eneo linalokaliwa na Wasunni wengi.