1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Baraza zima la mawaziri kubadilishwa Irak

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtC

Mashambulio nchini Irak yameua zaidi ya watu 40 na hadi 70 wengine wamejeruhiwa. Katika shambulio moja la kujitolea muhanga hadi watu 35 waliuawa kwenye kituo cha polisi cha kutoa ajira mjini Baghdad.Wakati huo huo,wanajeshi 4 wa Kingereza wameuawa na 3 wamejeruhiwa vibaya sana katika shambulio lililofanywa dhidi ya boti iliyokuwa ikipiga doria kwenye “Ujia wa Shaat al-Arab” katika mji wa bandari wa Basra kusini mwa Irak. Wanajeshi 3 wa Kimarekani pia wameuawa katika mapigano yaliyozuka katika wilaya ya Anbar. Mmuagiko wa damu ukiendelea nchini humo,waziri mkuu Nuri al-Maliki amesema anataka kulibadilisha baraza zima la mawaziri wake.Ofisi ya waziri mkuu imesema,vyeo vyote vitapangwa upya.Baada ya kikao cha bunge,al-Maliki alie madarakani tangu miezi sita,alitoa mwito kwa wanasiasa wa vyama vyote kushiriki katika utaratibu huo.