1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Ghasia zimeongezeka Iraq.

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIz

Hali ya ghasia nchini Iraq imepanda zaidi katika miezi miwili ya mwanzo ya mwaka huu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya wizara ya ulinzi ya Marekani ambayo inasema kuwa mashambulizi dhidi ya majeshi yanayoongozwa na Marekani na raia wa Iraq imefikia kiwango kibaya sana katika muda wa zaidi ya miaka mitatu.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mashambulizi kwa wastani kila wiki katika mwezi wa Januari na Februari imepita kiasi cha mashambulizi 1,000, ikilinganishwa na kiasi cha mashambulizi 900 katika muda wa miezi sita ya mwaka 2006.