1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Huenda Saddam akanyongwa mwishoni mwa juma hili.

29 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfI

Maafisa wa Marekani na Iraq wametoa taarifa za kutatanisha kuhusu siku ambayo Rais wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein anatarajiwa kutiwa kitanzi.

Afisa mkuu wa usalama wa Marekani amesema Saddam huenda akanyongwa kufikia siku ya jumamosi lakini maafisa wa Iraq wamekataa kuthibitisha iwapo Saddam atanyongwa katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Mtawala huyo wa zamani wa kiimla alihukumiwa adhabu ya kifo kwa mauaji ya mwaka elfu moja mia tisa themanini na mbili ya watu 148 katika mji wa Dujail, ambao wakazi wake wengi ni wa jamii ya kishia.

Kwa mujibu wa sheria ya Iraq hukumu hiyo inatakikana kutekelezwa katika kipindi cha siku thelathini.