1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Idadi ya vifo yumikini kufikia 500

16 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYj

Wafanyakazi wa uokozi wamekuwa wakiendelea hadi usiku wa manane hapo jana kufukuwa vifusi kutokana na milipuko mikubwa ya mabomu yaliotegwa kwenya malori manne kaskazini mwa Iraq karibu na mpaka wa Syria ambapo idadi ya vifo imekuwa ikizidi kuongezeka na yumkini ikafikia watu 500.

Idadi hiyo imekaririwa na kituo cha televisheni ya Kiarabu cha Al Jazeera na kile cha Marekani cha CNN kwa kuzingatia takwimu kutoka kwa madaktari wa eneo hilo,hospitali na maafisa wa serikali ya mitaa.

Mashambulio hilo hayo yaliotokea hapo Jumanne ambayo maafisa wa kijeshi wa Marekani wanawalaumu magaidi wa Al Qaeda kuhusika nayo yalilenga maeneo manne katika kijiji kilioko kilomita 120 kutoka mji wa Mosul.

Generali Kevin Bergner msemaji wa jeshi la Marekani anasema Al Qaeda inaendelea kuwa na uwezo wa kufanya mashambulizi hayo makubwa ya kushtuwana inaonyesha tabia ya adui ya kutojali kabisa maisha ya binaadamu na ukweli kwamba watafanya mambo hayo kuchochea umwagaji damu ili kutangazwa kwenye vyombo vya habari na kwa chochote kile kitakachoweza kutimiza dhamira yao.

Naye Meja Generali Benjamin Mixon wa Marekani amekiambia kituo cha televisheni cha CNN kwamba mauaji hayo karibu yanalingana na mauaji ya kimbari kwa sababu yamelenga dehehebu la Yazidi la kabila la Wakurdi.

Yazidi ni dhehebu la kidini ambapo wafuasi wake wako kaskazini mwa Iraq na wanaishi kwenye vijiji vilioko karibu na mji wa Mosul na hawafuati mafundisho ya Kiislam.

Mamia ya watu wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ya kujitolea muhanga maisha.