1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anusurika

22 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGT

Kombora limevurumishwa katika eneo ambako Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alikuwa akifanya mkutano na waandishi wa habari mjini Baghdad.

Picha televisheni zimemuonesha Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa akiinama chini ya meza baada ya kishindo kikubwa kusikika, lakini Waziri Mkuu wa Iraq, Noor Al Maliki alionekana kutokuwa na wasi wasi na kumwambia tulia.

Mkutano huo na waandishi wa habari, unafuatia ziara ya ghafla hii leo huko Iraq ya Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, na eneo alipokuwa akifanya mkuitano huo lina ulinzi mkali wa majeshi ya Marekani.

Bila ya kuzungumzia lolote kuhusiana na shambulizi hilo, Ban Ki Moon aliendelea kujibu maswali ya waandishi wa habari.

Ziara hiyo huko Baghdad imekuja huku kukiwa na taarifa za kuawa kwa askari watatu wa Marekani katika mji wa Basra.