1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Kesi ya wafuasi wa Saddam Hussein yaanza tena leo

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBN1

Kesi inayowakabili wasaidizi 15 wa aliyekuwa rais wa Irak Sadam Hussein imeanza hii leo katika mahakama mjini Baghdad chini ya ulinzi mkali.

Ali Hassan al Majid kwa jina maarufu Kemikal Ali ambae ni binamu yake Saddam Hussein anaekabiliwa na adhabu ya kifo baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya halaiki katika kesi nyingine, ametaka kesi hiyo ya uhalifu dhidi ya binadamu inayomkabili pamoja na wenzake 14 iahirishwe kwa muda wa mwezi mmoja.

Kemikal Ali alimueleza jaji Mohamed al Khalifa al Oreibi kuwa yeye na wenzake wanahitaji muda huo ili mawakili wanaowatetea waweze kuendelea kuhudhuria shughuli za mahakama baada ya ombi lao la kutaka ulinzi kutoka kwa kikosi cha Marekani kukataliwa.

Mawakili hao wanahofia usalama wao.