1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Kunyongwa kwa wasaidizi wa Saddam kumeahirishwa

5 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdH

Maafisa wa Iraq wameahirisha kunyongwa kwa wasaidizi wawili wa zamani wa dikteta aliyepinduliwa wa nchi hiyo Saddam Hussein yumkini hadi hapo Jumapili.

Kaka wa kambo wa Saddam na hakimu mkuu wa mahkama ya kimapinduzi walikuwa wakitazamiwa kunyongwa hapo jana Alhamisi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na Mkuu wa Haki za Binadaamu wa Umoja wa Mataifa Louise Arbour wamemsihi moja kwa moja Rais Jalal Talabani wa Iraq kutowanyonga watu hao.

Wakati huo huo walinzi wawili wamekamatwa kwa kuhusika kwao katika kuvuta kwa siri filamu ya kunyongwa kwa Saddam na baadae kusambazwa kwenye mtandao.