1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Maafa ya mabomu yaendelea Iraq.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuJ

Mabomu yaliyotegwa kwenye magari mawili yalilipuka kwa wakati mmoja na yakaua watu saba na wengine ishirini na saba wakajeruhiwa kaskazini mwa Baghdad.

Milipuko hiyo imetokea katika mtaa wa Kadhimiya ulio na wakazi wengi wa madhehebu ya Shia katika eneo linaloishi waumini wa madhehebu yote mawili ya Shia na Sunni.

Serikali ya Waziri Mkuu, Nuri al-Maliki inajitahidi kuanzisha tena mchakato uliokwama wa maridhiano ya kitaifa nchini Iraq lakini mzozo wa kimadhehebu nchini humo unatatiza juhudi hizo.

Kwengineko, mjini Najaf kusini mwa Iraq watu watatu wasiojulikana wamemuua kwa kumpiga risasi mwakilishi wa kiongozi mkuu wa kishia, Ayatollah Ali al-Sistani.