1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Maafa ya mabomu yaendelea Iraq

13 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2Q

Watu zaidi ya arobaini wameuawa na wengine kama miammoja wamejeruhiwa baada ya mashambulio ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari.

Katika eneo la kaskazini linalokaliwa na wakurdi wengi, watu takriban thelathini wamefariki baada ya mtu wa kujitoa mhanga kulipua bomu kwenye gari karibu na afisi za serikali katika mji wa Makhmour.

Watu kama hamsini wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Kwenye eneo la kati la Baghdad, watu kumi na mmoja wamefariki na wengine arobaini na watatu wamejeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari karibu na soko.

Mashambulio hayo yametekelezwa wakati ambapo wanajeshi kiasi elfu nne wa Marekani wanaendelea kuwatafuta wenzao watatu waliotekwa nyara jana kusini mwa Baghdad.

Kundi moja linalohusishwa na mtandao wa al-Qaeda limetangaza kwenye ukurasa wake wa tovuti kwamba linashikilia wanajeshi hao watatu.